Mabingwa wa soka Tanzania Bara Simba huenda wakaweka kambi nchini Afrika Kusini kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu ya Tanzania Bara pamoja na michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, imefahamika
Awali Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba Mohammed Dewji 'Mo' alipendekeza timu hiyo kuweka kambi moja ya nchi barani Ulaya
Hata hivyo baada ya majadiliano, kuweka kambi Afrika Kusini kumeonekana kutaipa manufaa zaidi Simba kulekea msimu ujao
Simba inatarajiwa kuelekea Afrika Kusini ndani ya kipindi cha wiki mbili ambapo kocha Mkuu Patrick Aussems atakuwa amerejea
Hii haitakuwa mara ya kwanza kwa Simba kuweka kambi Afrika Kusini. Mwaka juzi kambi ya timu hiyo ilikuwa hukohuko Bendeni
No comments:
Post a Comment