We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Tuesday, July 2, 2019

KESI YA MEMBE, MAHAKAMA KUU YAMPA SIKU 7 MUSIBA

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imempa siku saba mmiliki wa gazeti la Tanzanite, Cyprian Musiba na wachapishaji wa gazeti hilo, wawe wamewasilisha majibu dhidi ya madai ya aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje, Bernard Membe,  anayetaka kulipwa Sh bilioni 10 kwa kuchafuliwa.

Uamuzi huo wa mahakama umetolewa leo Jumanne Julai 2, mbele ya Jaji Joaquine Demelo baada kupitia maombi ya wajibu maombi ya kutaka waongezewe muda wa kuwasilisha utetezi na majibu kinzani.

Jaji Demelo amesema wajibu maombi walitakiwa kuwasilisha utetezi na majibu kinzani ndani ya siku 21 baada ya shauri kufunguliwa Desemba mwaka jana lakini hawakufanya hivyo ambapo Musiba kupitia wakili wake Majura Magafu waliomba kuongezewa muda japo wadai walipinga maombi hayo wakitaka yasikubaliwe.

“Mahakama imesikiliza hoja za pande zote mbili imeona kesi ina maslahi kwa umma hivyo ni bora na upande mwingine wakasikilizwa. Hatuwezi kusikiliza shauri upande mmoja, kesi hii ina maslahi kwa umma,  kuna haja ya kuusikiliza na upande wa pili; nawapa siku saba muwasilishe utetezi na hati ya kiapo kinzani,” amesema Jaji Demelo.

Jaji Demelo alisema upande wa waleta maombi kama watakuwa na hoja za kujibu utetezi wawasilishe kabla ya Agosti 8, mwaka huu ambapo shauri hilo la madai litaanza kusikilizwa Agosti 6, mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list