Kikosi cha Simba kiko Afrika Kusini kikiendelea na maandalizi ya msimu mpya wa ligi kuu ya Tanzani Bara pamoja na michuano ya ligi ya mabingwa na mingineyo
Kesho Jumanne, Julai 30 2019 Simba itamaliza mchezo wa mwisho wa kujipima huko Afrika Kusini kwa kuumana na mabingwa wa Curling Cup, Orlando Pirates
Juzi Pirates ilitwaa taji hilo kwa kuichapa Kaizer Chiefs mabao 2-0
Simba inatarajiwa kurejea nchini mwishoni mwa wiki hii tayari kwa tamasha la Simba Day litakalofanyika August 06 kwenye uwanja wa Taifa
Simba ilitua Afrika Kusini Julai 17 ambapo imecheza michezo mitatu ya kirafiki
Mabingwa hao wa nchi walianza kwa kuilaza Orbit Tvet mabao 4-0, wakaichapa Platinum Stars mabao 4-1 kabla ya kulazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Township Rollers juzi
Baada ya mchezo wa juzi, kocha Aussems alisema vijana wake wameiva

No comments:
Post a Comment