Beki wa kushoto wa Yanga Gadiel Michael bado hajasaini mkataba mpya wa kuitumikia timu hiyo licha ya makubaliano kufikiwa
Uongozi wa Yanga unaweza kuachana na beki huyo kama ataendelea kuwasumbua mabosi wa Kamati ya usajili ambao juzi walishindwa kumalizana nae nchini Misri
Inaelezwa Yanga imemtaka Gadiel asaini mkataba wake kabla ya Ijumaa ya wiki hii
Kinyume na hivyo huenda akaondolewa kikosini kulingana na maagizo yaliyotolewa na kocha Mwinyi Zahera
Kumekuwa na tetesi kuwa Gadiel ameungana na Ibrahim Ajib kutua kunako klabu ya Simba
Baada ya kufikiwa makubaliano, uongozi wa Yanga ulimpa Gadiel mkataba asaini kabla hajaondoka kwenda Misri
Hata hivyo viongozi wa Kamati ya usajili walipokwenda Misri kumalizana na baadhi ya wachezaji, walibaini kuwa Gadiel hakuwa ameusaini mkataba aliokaa nao kwa zaidi ya wiki mbili
Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla amempa Gadiel masaa 24 awe ameusaini mkataba huo la sivyo jina lake litaondolewa kwenye kikosi cha Yanga

No comments:
Post a Comment