We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Friday, July 5, 2019

Serikali kufufua viwanda vilivyokufa Kilimanjaro

Serikali imeanza  utekelezaji wa kufufua  kiwanda cha kutengeneza vipuli  vya viwandani  na magari  cha Mashine tools kilichopo wilayani Hai mkoani Kilimanjaro, ambacho kilisimamisha uzalishaji kwa zaidi ya mika 30.
Waziri wa viwanda na biashara Innocent Bashunga amethibitisha jambo hilo jana Alhamisi Julai 4, wakati wa akizindua matengenezo ya tela za trekta mpya katika kiwanda hicho ambapo amezitaka taasisi zinazotengeneza  zana za viwandani kuzalisha bidhaa bora zitakazowasaidia wakulima wadogo ili kufikia malengo ya serikali ya uchumi wa viwanda.
Amesema kuwa tayari serikali imeridhia ombi la Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro la kufufua viwanda ambavyo vimekufa kwa muda mrefu na kwamba lazima mkakati huo uende sambamba na kubadilisha maisha ya wakulima wadogo.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Anna Mghwira, amesema mpango wa kufufua kiwanda hicho kitakuwa mkombozi mkubwa kwa wananchi mkoani humo na kwamba kuna wawekezaji kutoka nje ambao wameonyesha nia ya kuja kuwekeza katika kiwanda hicho.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list