Rapper 50 Cent ameingia kwenye headline kwa mara nyingine, hii ni baada ya kumkana hadharani kijana aitwaye Marquise Jackson (21) anayedaiwa kuwa ni mtoto wake.
50 Cent kupitia ukurasa wake wa Instagram, amesema kuwa kijana huyo sio mtoto na tayari ameshapima damu kuhakikisha hilo.
“Yule sio mtoto wangu, Nimeshapima damu. Nitolee umbumbavu wako hapa,“ameeleza 50 Cent kwa kumjibu shabiki yake ambaye aliuliza kwanini? 50 Cent kwenye show yake na Snoop Doggy walimbania dogo Marquis Jackson asiingie backstage na kumuacha nje kwenye viti vya kawaida.
Mwaka jana kijana Jackson, aliposti picha na akiwa na mtoto wa Supreme McGriff ambaye ni hasimu wa 50 Cent kwa muda mrefu, Jambo hilo lilimkwaza mkali huyo wa Hip Hop na akashindwa kuzuia hisia na kukomenti kwenye post hiyo kwa kuandika, “Hata kama watu hawa wawili wakigongwa na gari, Kwangu haitakuwa siku mbaya,“.
No comments:
Post a Comment