Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba Crescentius Magori amesema klabu hiyo imedhamiria kumbakisha mshambuliaji wake kutoka Uganda Emmanuel Okwi
Magori amesema bado mazungumzo ya kumuongezea mkataba yanaendelea na kila kitu kitaweka hadharani baada ya kufikiwa makubaliano
Okwi yuko nchini Misri na kikosi cha timu ya Taifa ya Uganda, akiwa amefunga mabao mawili kwenye michuano ya Afcon inayoendelea nchini humo
Hata hivyo kutokana na kufanya vizuri kwenye michuano hiyo, Simba italazimika kumuongeza dau la usajili/mshahara kwani inaelezwa timu nyingi zimejitosa kumuwania
No comments:
Post a Comment