We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Monday, July 8, 2019

Rais Magufuli amtumia salamu za rambirambi Bakhresa “Nimeshtushwa sana”

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Mwenyekiti wa Kampuni za Said Salim Bakhresa kufuatia vifo vya wafanyakazi 5 wa vyombo vya habari vya Azam Media Limited vilivyotokea leo tarehe 08 Julai, 2019 katika ajali ya barabarani. 
Ajali hiyo imetokea majira ya saa 2:30 asubuhi katika eneo la Kizonzo, katikati ya Igunga (Tabora) na Shelui (Singida) ambapo basi aina ya Coaster lililowabeba wafanyakazi wa Azam Media Limited likielekea Mwanza limegongana uso kwa uso na Lori la mizigo lililokuwa linakwenda Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Azam Media Limited walikuwa safarini kutoka DSM kuelekea kwenye sherehe za uzinduzi wa Hifadhi ya Taifa ya Burigi-Chato kwa ajili ya kurusha matangazo ya moja kwa moja ya sherehe hizo.
Katika salamu hizo, Rais Magufuli ameelezea kushtushwa na taarifa za ajali iliyosababisha vifo vya watu 7 wakiwemo wafanyakazi hao 5, Dereva na Msaidizi wake na amewaombea Marehemu wote wapumzike mahali pema peponi, Amina.
“Nimeshtushwa sana na vifo hivi, nampa pole Mwenyekiti Ndg. Said Salim Bakhresa, ndugu wa Marehemu wote, Mtendaji Mkuu Ndg. Tido Mhando na wafanyakazi wote wa Azam Media Ltd, waandishi wa habari wote na watu wote walioguswa na vifo hivi” Rais Magufuli. 
Rais Magufuli amewaombea majeruhi 3 wa ajali hiyo wapone haraka ili waweze kuendelea na majukumu yao ya kila siku.
Aidha, Rais Magufuli amerejea wito wake wa kuwataka watumiaji wa barabara hususani madereva kuwa makini na kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepusha ajali zinazoweza kuepukika.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list