Uongozi wa Simba bado haujamaliza michakato ya usajili ambapo inaelezwa zoezi liko kwenye hatua za mwisho
Mpaka sasa Simba tayari imetumia zaidi ya Bilioni 1.3 kusajili nyota wapya na kuwaongezea mikataba wengine
Ni dhahiri Simba itavuka kiwango kilichotumiwa kusajili msimu uliopita ambapo Bilioni 1.3 zilitumika
Mtendaji Mkuu wa Simba Crescentius Magori amesema baada ya kukamilisha zoezi la usajili, wataweka hadharani kiasi cha fedha zilizotumika
Simba ilitenga bajeti ya Bilioni 2.6 kwa ajili ya usajili

No comments:
Post a Comment