We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Friday, July 12, 2019

Prof. Kitila Mkumbo azungumzia kuhusu kugombea Ubunge

Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Profesa Kitila Mkumbo amezungumzia suala la kugombea Ubunge katika Uchaguzi Mkuu mwaka 2020.


Akizungumza na EA Radio, Prof. Mkumbo amesema kuwa kwa sasa anatekeleza majukumu aliyokabidhiwa na Rais Magufuli kuhakikisha kuwa maji yanatoka maeneo mbalimbali nchini na ikifika wakati husika ataamua endapo atagombea ama vinginevyo.
"Suala la Ubunge kwa sasa bado, ninachapa kwanza kazi aliyonikabidhi Rais Magufuli. Imebaki miezi 12 ya kujua hatma na maamuzi ya endapo nitagombea ama vinginevyo", amesema Prof. Mkumbo.
Pia amezungumzia juu ya kero sugu za maji zinazosumbua maeneo mbalimbali ya Jiji la Dar es salaam kama Gongo la mboto, Chanika, Goba na maeneo mengine ambayo miradi haijakamilika, ambapo amesema mchakato wa kukamilisha miradi hiyo unakwenda kwa kasi na ndani ya miezi 12 ijayo wananchi wataanza kutumia maji.
"Wananchi wa Dar es salaam na maeneo mengine nchini wasiwe na wasiwasi, serikali inaendelea kutekeleza ilani ya CCM kwa ufanisi, mpaka kufikia April mwaka huu tumeweza kuwasambazia maji wanannchi kwa asilimia 65 na malengo yetu mpaka mwisho wa 2020/21 tutakuwa tumewafikia wananchi kwa asilimia 85", ameongeza.
Profesa Kitila Mkumbo alikuwa mshauri wa Chama cha ACT-wazalendo kabla ya kuteuliwa na Rais Magufuli, April 04, 2017 kuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji ambayo bado anahudumu mpaka sasa.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list