Beki aliyemaliza mkataba kunako klabu ya Yanga Abdallah Shaibu 'Ninja' yuko kwenye hatua za mwisho kujiunga na klabu ya Solvakia, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Czech
Hata hivyo Solvakia huenda ikamtoa kwa mkopo kwenda klabu ya LA Galaxy ya Marekani
LA Galaxy ndio timu anayocheza nyota wa zamani wa PSG na Manchester United, Zlatan Ibrahimovich
Licha ya kuanza kwa kusuasua Yanga, Ninja alionyesha ukomavu kwenye mwaka wa pili wa mkataba wake ambapo msimu uliopita ndiye beki aliyecheza mechi nyingi zaidi kwenye kikosi cha Yanga
Bado angehitajika zaidi kwenye kikosi cha Yanga lakini uwezekano wa kubaki umezidi kuwa mdogo hasa baada ya kupata ofa iyo nono ambayo ikimtokea mchezaji inakuwa ndoto iliyotimia kwake
No comments:
Post a Comment