We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Friday, July 26, 2019

Nimeridhishwa na usajili uliofanyika - Aussems

Kocha Mkuu wa Simba Patrick Aussems amesema ameridhishwa na viwango vya wachezaji wapya waliosajiliwa na timu hiyo na anaamini muda wa kutengeneza timu imara bado upo
Akizungumzia usajili wa wachezaji wapya,  Aussems amesema aliwaachia viongozi wa Simba orodha ya wachezaji nane/tisa aliotaka wasajiliwe
Ingawa sio wote waliosajiliwa,lakini anaamini waliopo wana ubora
"Kuhusu wachezaji wapya, kabla sijaondoka kwenda mapumziko, niliacha orodha ya majina ya wachezaji nane au tisa ambao nilitaka wasajiliwe," amesema
"Mmoja wapo ni huyu Msudani (Shiboub) na hawa Wabrazil watatu. Bila ya kujali kilichotokea, mpaka sasa nimeridhishwa na ninachokiona mazoezini"
"Lakini huu ni mwanzo wa maandalizi yetu, bado tunafanya kazi"
"Mimi napenda kuwa muwazi, baadhi ya wachezaji ambao niliwahitaji sikuwapata japo mpaka sasa nimeridhishwa na hawa waliopo, wanafanya vizuri..tusubiri tuone baadae"
Simba imeongeza nyota wapya 11 kwenye kikosi chake kwa ajili ya msimu ujao
Wachezaji wazawa waliotua Simba ni Beno Kakolanya, Kennedy Juma, Ibrahim Ajib, Gadiel Michael na Miraji Athumani
Wachezaji wa kigeni waliosajiliwa ni Tairone Santos da Silva, Wilker Henrique da Silva, Gerson Fraga Viera, Shariff Elden Shiboub, Deo Kanda na Francis Kahata
Simba bado ina nafasi moja ya kukamilisha idadi ya wachezaji 10 wa kigeni

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list