Kauli hiyo imetolewa baada ya baraza hilo kupokea malalamiko ya wananchi kuwa baa na kumbi hizo za starehe zinapiga muziki kwa sauti kubwa.
Hayo yameelezwa leo Jumatano Julai 24, 2019 katika mkutano wa baraza hilo uliolenga kuwaelimisha wamiliki wa baa na kumbi za starehe na sherehe namna ya kuepukana nazo.
Akizungumza katika mkutano huo, Mkurugenzi wa NEMC, Dk Samuel Gwamaka amesema katika kipindi cha mwezi mmoja uliopita alipokea zaidi ya malalamiko 100 ya kelele kutoka kwa wananchi.
“Sasa kelele hizo zina athari mbalimbali kwa jamii iliwemo kusababisha magonjwa sababu kitu chochote unachokifanya wewe siyo wote wanakifurahia,” amesema
Amesema kama baraza pia linahusika katika utoaji wa vibali vya matamasha mbalimbali kwa kuzingatia muda maalumu wa kufanyika kwa tamasha hilo, kiwango cha kelele kitakachozalishwa.
Naye Meneja wa Tips bar iliyopo Mikocheni, Dar es Salaam, Ismail Kagambo amesema elimu hiyo ilipaswa kutolewa miaka mingi nyuma ili wajue namna wanayoweza kuepuka hali hiyo.
“Huwa tunapokea malalamiko mengi kutoka kwa majirani zetu, tumekuwa tukikaa nao na kuwaeleza hali halisi lakini pia Nemc inapaswa kupita na kwa jamii inayotunguka kuwapitia elimu hii,” amesema Kagambo.

No comments:
Post a Comment