Akizungumza jijini Mwanza leo Jumatatu Julai Mosi, 2019, Naibu Waziri Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Tanzania, Atashasta Nditiye amesema mchakato huo utakamilika muda wowote kuanzia sasa.
Naibu Waziri huyo alikuwa anafungua mkutano wa siku tano wa wataalam wa mawasiliano kutoka mamlaka za mawasiliano za wanachama wa EAC.
Tanzania na Burundi ndizo nchi pekee kati sita wanachama wa EAC ambao hawajakamilisha mchakato huo.
Nchi za Kenya, Rwanda, Uganda na Sudan Kusini tayari zimeoanisha gharama za simu ikiwa ni utekelezaji wa mkataba wa EAC kuhusu sekta ya mawasiliano ya simu.
"Tuko hatua za mwisho kukamilisha mchakato wa kuoanisha gharama za kupiga simu miongoni mwa nchi wanachama wa EAC," amesema Nditiye
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA), James Kilaba amewaeleza washiriki kuwa licha ya Tanzania kutokamilisha mchakato huo, sera za mawasiliano nchini ndizo zilizo bora kulinganisha na mataifa mengine wanachama wa EAC.
Amesema sababu zinahusisha huduma na manufaa kwa asilimia 94 ya wananchi wote hadi vijijini.
"Sera za Tanzania ndizo zimeigwa na EAC kutokana na ubora wake na upatikanaji wa mawasiliano vijijini," amesema Kilaba
Kwa upande wake, Mtendaji wa Shirika la Mawasiliano wa EAC, Ally Simba amesema lengo la kuoanisha gharama za mawasiliano miongoni mwa raia wa nchi wanachama kurahisisha mawasiliano.
No comments:
Post a Comment