Leo July 29, 2019 Mbunge wa Mtama Nape Nnauye amefanya mkutano wa hadhara katika Jimbo lake na kuzungumza juu ya zao la Korosho ambalo kwa asilimia kubwa linalimwa Mikoa ya kusini mwa Tanzania.
“Kazi yangu kuhakikisha watu wangu wanalipwa na mimi matumaini yangu baada ya muda huu wa milima na mabonde Serikali wamejifunza watarekebisha mambo, ninayo matumaini kwamba Korosho iliyopo kama bado nzima itapata soko, ni matumaini yangu juhudi zinazofanywa na Serikali kuiondoa hiyo korosho zitanyike mapema maana isipotoka korosho mpya haina pa kukaa” – NAPE
No comments:
Post a Comment