Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla amesema timu hiyo ina thamani kubwa na hawatakubali iyumbishwe na mchezaji mmoja
Akizungumzia hatma ya beki Gadiel Michael, Dk Msolla amesema wamempa muda wa kuamua kama anataka kubaki Yanga au la
Jana Dk Msolla alimtaka mchezaji huyo akamilishe usajili wake ndani ya masaa 24
Hata hivyo Gadiel yuko na timu ya Taifa nchini Misri ambapo kikosi hicho kinatarajiwa kuwasili nchini kesho Alhamisi baada ya kuondoshwa hatua ya makundi michuano ya Afcon 2019
"Suala la Gadiel halitusumbui, kuna wachezaji wengi sana, tumemtaka asaini mkataba atakaporejea au sivyo aseme tumruhusu aondoke," amesema
"Yanga ni taasisi kubwa, hakuna mchezaji wala kiongozi ambaye ni mkubwa kuliko taasisi hii"
"Sio jambo jema kumsumbua mwajiri wako hivyo tumemwambia aamue."
"Hatutasikitika akiondoka, lakini atakuwa ametupotezea muda wa kuweza kusajili mchezaji wa kuchukua nafasi yake"
Inaelezwa Gadiel alishafikia makubaliano ya kuongeza mkataba wa kuendelea kubaki Jangwani
Lakini imebainika, hakuusaini mkataba aliopewa na uongozi wa Yanga kabla ya kwenda Misri kushiriki Afcon
Imeelezwa mpaka Ijumaa kama mchezaji huyo hatakuwa amesaini, ataondolewa kukosini na nafasi yake inaweza kuchukuliwa na David Kuhende au Shafiq Batambuze
Yanga inatarajiwa kuanza mazoezi ya maandalizi ya msimu mpya wiki ijayo, hivyo imedhamiria kukamilisha usajili mapema

No comments:
Post a Comment