We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Sunday, July 28, 2019

Mkwabi akimbilia polisi

WAKATI wanachama na mashabiki wa Simba wakiwa njiapanda juu ya hatma ya Bilionea wa klabu hiyo, Mohammed ‘Mo’ Dewji, baada ya serikali kutoa maelekezo mapya ya suala la uwekezaji ndani ya klabu za soka za wananchi, mambo ya Msimbazi yamezidi kutibuka.
Hii ni baada ya kubainika kuna mtu analitumia jina la Mwenyekiti wa Simba, Swedy Mkwabi kutibua mambo kwa wiki kadhaa tangu sakata ya Mo Dewji kutishia kujitoa Simba na kueleza anakwamishwa na Mkwabi katika kukamilisha mchakato kwa kuigeuza Simba kuwa kampuni.

Sakata hilo ndilo lililomuibua Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe kutoa tamko majuzi klabu zote za soka zinazotaka kuingia kwenye mfumo wa hisa kuzingatia matakwa ya kisheria na kanuni inatotoa nafasi kwa Hisa 49 kumilikiwa na wawekezaji na sio mwekezaji kama ilivyo Simba kwa sasa.
Tamko hilo la Dk Mwakyembe ni matakwa ya kanuni namba 18 iliyofanyiwa marekebisho na Baraza la Michezo (BMT) ambayo waziri huyo aliisaini Septemba 21, 2017, lilimfanya aliyekuwa Mwenyekiti wa Baraza la Wadhamini wa Simba, Hamis Kilomoni kuibuka na kuitisha mkutano juzi nyumbani kwake kabla ya polisi kuingilia kati na kumkamata.
Lakini wakati mgogoro ukiendelea na kuwagawa wanachama na mashabiki wa Simba, kuna akaunti moja ya instagramu yenye jina la Swedy Mkwabi imekuwa ikichocheza zaidi kwa kuposti kauli tata, lakini Mwenyekiti wa klabu hiyo ameikana akidai siyo yake.
Mkwabi alisema tayari aliwasiliana na wenzake Simba na kupeleka taarifa Polisi na vyombo vingine kumsaka jamaa huyo anayewavuruga kipindi ambacho Simba inahitaji umoja na mshikamano.
Akaunti hiyo inayotumia jina la Swedimkwabi ilionyesha kuandikwa ‘maelekezo ya Mwakyembe yanafaa kufanyiwa kazi kwa haraka kwa ajiri ya afya ya timu yetu’.

Mkwabi alipotafutwa jana alisema; “Ni lazima nichukue hatua maana hii sio jambo zuri kwangu ndani ya klabu, wananichafulia kwa kutumia jina langu vibaya, nitakwenda TCRA na sehemu nyingine ambazo zinahusika na masuala ya makosa ya kimtandao ili wachukue hatua stahiki.
“Hata picha zilizowekwa katika akaunti hiyo si zangu ambazo nimeziposti, ni picha za mitandao, akaunti yangu halisi ni sweddymkwabi na si swedimkwabi, mara ya mwisho kuposti kwenye akaunti yangu ni Julai 11, 2018 yote hiyo ni kwa vile mi si mtu wa kushinda mitandaoni, huyo ni mtu ameamua kutafuta vurugu na kuwachanganya Wanasimba.”
Kuhusu kauli ya waziri alisema; “Tuna kikao cha Bodi ya Wakurugenzi ambacho kitakaa siku yoyote kuanzia sasa, tutajadili mbambo mbalimbali likiwemo hilo tamko la Waziri ndipo tutalitolea tamko,”
AMVAA MDOGO WAKE
Miongoni mwa tuhuma ambazo Mkwabi analalamikiwa ni madai ya kuwa karibu na Mzee Kilomoni anayedaiwa kukataa kutoa hati ya klabu hiyo sambamba na Katibu wake wa Baraza la Wazee, Fikirini Mkwabi ambaye wamekuwa wakilalamikia mabadiliko mabovu ya mfumo wa klabu yao.
Mkwabi alisema anaumia na kinachofanywa na ndugu yake na kuongeza; “Fikirini ni ndugu yangu na hii ishu inayoendelea na Mzee Kilomoni akishirikiana naye ni hali ambayo inaivuruga klabu na familia yetu, nimejaribu kumsihi kuachana na mambo hayo lakini imekuwa vigumu kuelewa matokeo yake naonekana mimi miongoni wazalisha vurugu.”

“Wanasimba waelewe tu kinachoendelea hakihusiani na mimi kikubwa tutulie maana bodi inajadili mwenendo mzima wa kila kinachoendelea sasa,” alisema.
AUSSEMS AJA NA YAKE
Katika hatua nyingine, Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems alisema amevutiwa na namna Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba na viongozi wengine walivyosimamia mchakato wa usajili wa klabu hiyo iliyopo Afrika Kusini kwa sasa.
Aussems alisema kulingana na ripoti yake baada ya msimu kumalizika wachezaji ambao alikuwa anawahitaji wengi wao wamepatikana, pia hata maboresho ya benchi la ufundi yamefanyika ambayo yalikuwa muhimu kulingana na kucheza mashindano mfululizo.
“Niupongeze uongozi kwa kuipeleka timu mahala sahihi kwa kwenda kufanya maandalizi ya msimu hapa Afrika Kusini kwani hapa tunapata kila kitu na kufanya mazoezi kwa wakati kama vile ambavyo benchi la ufundi tumepanga.
“Kiujumla kambi ina maendeleo mazuri kwa kiasi kikubwa mambo mengi ambayo benchi la ufundi lilihitaji kufanya tumefanikiwa kuyafanya na tunaendelea na ratiba nyingine kwa muda uliobaki kabla ya kurudi nyumbani.”

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list