Mbunge huyo wa Vunjo ametoa kauli hiyo jana asubuhi Julai 27, 2019 katika mkutano mkuu wa NCCR Mageuzi unaofanyika jijini Dar es Salaam.
“Mimi naona wewe unataka kuongoza hivi, mimi nina mawazo mbadala ya kuweza kuboresha hili kwa ajili ya maendeleo endelevu ya watanzania ndiyo maana ya upinzani. Kunapokuwa na changamoto ya upinzani. Taifa linaneemeka zaidi.”
“Ndiyo maana leo kutoka sakafu ya moyo wangu huu upinzani tunasema si uadui, lazima tukubaliane. Mabadiliko yote yanaanza katika mabadiliko ya kifikra,” amesema Mbatia.
Katika hatua nyingine, Mbatia ametumia jukwaa hilo kuwaomba radhi Watanzania baada ya chama hicho kuwa kimya kwa muda mrefu bila kuonyesha mbwembwe zozote.
“Tulijitafakari na tafakari yetu hadi jana kuhusu mabadiliko katika fikra. Niwe mkweli mimi sijazaliwa kuwa mwenyekiti wa kudumu wa NCCR Mageuzi. Ningetamani kuona mwanamke ili kutekeleza kwa vitendo malengo ya kidunia,” amesema.

No comments:
Post a Comment