Ukimuondoa Farouq Shikalo ambaye atajiunga na Yanga baada ya mchuano ya Kagame kumalizika, Mshambuliaji Sadney Urikhob ndiye pekee ambaye hakuwa ameripoti kwenye kambi ya timu hiyo mkoani Morogoro
Uongozi wa Yanga umethibitisha kuwa mshambuliaji huyo yuko njiani na kesho ataungana na wachezaji wengine mkoani Morogoro
Urikhob ni miongoni mwa nyota wapya nane wa kigeni waliosajiliwa na Yanga kwa ajili ya msimu ujao
Wengine ni Farouk Shikalo, Mustafa Suleyman, Lamine Moro, Patrick Sibomana, Issa Bigirimana, Juma Balinya na Maybin Kalengo
Kalengo, Moro, Sibomana, Bigirimana, Balinya na Mustafa tayari wako mkoani Morogoro

No comments:
Post a Comment