August 04 ndio kilele cha wiki ya Mwananchi ambayo itahitimishwa uwanja wa Taifa kwa mchezo wa kirafiki kati ya Yanga dhidi ya AS Vita Club kutoka DR Congo
Kabla ya tukio hilo kubwa, Wanafamilia wa Yanga watafanya shughuli mbalimbazli za kijamii katika maeneo wanayoishi
Shughuli zitakazofanyika kuanzia Julai 27 ni pamoja na kuzuru kaburi la hayati Mzee Karume, kupanda miti na kufanya usafi, kutembelea wagonjwa, kuchangia damu na kutembelea yatima
August 04 ndio hitimisho la matukio yote hayo kwa tukio kubwa kufanywa katika dimba la Taifa
Miongoni mwa matukio yatakayojiri siku hiyo ni kutambulisha wachezaji wapya, burudani ya muziki, kuzindua wimbo maalum wa Yanga na kutambulisha jezi za msimu mpya

No comments:
Post a Comment