Mchezo wa kirafiki kati ya Simba dhidi ya Township Rollers uliopigwa huko Afrika Kusini, umemalizika kwa timu hizo kufungana bao 1-1
Mchezo huo ulikuwa maalum kupima vikosi vya timu hizo ambazo zote zimeweka kambi Afrika Kusini kujiandaa na msimu mpya
Meddie Kagere aliitanguliza Simba kwa bao safi kwenye dakika ya 58 kabla Rollers hawajasawazisha kwenye dakika ya 70 kupitia kwa Serameng
Huo ni mchezaji wa tatu wa kirafiki kwa Simba ambayo iko Afrika Kusini tangu Julai 17
Imebakisha mchezo mmoja dhidi ya Orlando Pirates ambao utapigwa Julai 30 na baadae mabingwa hao wa Tanzania Bara kurejea nchini tayari kwa Tamasha la Simba Day litakalofanyika August 06

No comments:
Post a Comment