Ndoto ya Simba kumiliki uwanja wake wa mazoezi inaelekea kukamilika kutokana na uwekezaji wanaoufanya katika uwanja wake wa Bunju.
Picha mbalimbali zimeonesha hatua iliyopo katika uwanja huo hivi sasa, huku mafundi wakiwa katika hatua za mwisho za kuweka mabomba ya kupitisha maji katika uwanja.
Pia hatua nyingine inayofanyika hivi sasa ni ya kusambaza udongo katika eneo la kuchezea 'Pitch' kabla ya kuweka nyasi.
April 5, 2019, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa klabu ya Simba, Mohamed Dewji 'Mo' alidokeza kuwa kila kitu kimekamilika kutoka kwa mamlaka za serikali na kilichobaki sasa ni klabu kukamilisha na kuanza kuutumia uwanja huo kwa ajili ya mazoezi
Alisema kuwa ifikapo mwezi Mei watakakuwa katika hatua nzuri ya kuutumia uwanja huo, lakini mpaka sasa bado uko katika hatua za ujenzi na dalili za kukamilika kwa mwezi huu wa Julai ni ndogo.
No comments:
Post a Comment