Aliyekuwa kaimu katibu mkuu Yanga SC Omary Kaaya ameaga rasmi kuachia ofisi hiyo baada ya mkataba wake kutamatika rasmi tarehe 01 July 2019.
Wiki mbili zilizopita Kaaya alikutana na viongozi wa Yanga nakuwaeleza nia yake yakutoongeza mkataba wa kuitumikia klabu hiyo ili kuruhusu mawazo mapya pia changamoto mpya kwa yule atakayekuja badala yake.
Uongozi wa Yanga chini ya mwenyekiti wa klabu hiyo Mshindo Msolla uliridhia na kumchagua afisa habari wa klabu hiyo ndugu Dismasi Ten kushika kukaimu nafasi hiyo kwa muda mpaka hapo atakapopatikana Katibu mkuu mpya kutokana na ajira mpya walizotangaza Yanga SC hivi karibuni.
Dismasi Ten anatarajiwa kushika rasmi ofisi hiyo kuanzia leo tarehe 01 July 2019.
Kaaya atakumbukwa kwa mengi Yanga SC likiwemo suala la ushawashi kwa wanachama wa klabu hiyo kuichangia klabu hiyo.
KUBWA KULIKO ni moja ya mawazo yake ambayo yameipa thamani kubwa klabu hiyo na kuipa msingi wa uchumi bora kwa msimu ujao.
KUBWA KULIKO imeipa Yanga SC takribani bilioni 1.2 fedha za michango kutoka kwa watu na makampuni mbalimbali pia uwanja wa heka 7 eneo la Kigamboni , uwanja ambao Yanga walipewa na mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam mh. Paul Makonda.
Wakati Kaaya akipambana kwenye vyombo vya habari sanjali na wanachama wandamizi wapo walioibuka na kutaka kumvunja moyo kwa kusema Yanga haiwezi kuchangiwa kwa mfumo huo kama wachangiaji wa harusini lakini leo hii matunda yake yanaonekana kwa usajili mzuri na kuwafungulia njia nzuri viongozi wapya waliokuja katika njia mbadala yakujipatia fedha.
Haya ni machache amabyo yatawafanya wanayanga kumkumbuka kiongozi huyu aliyethubutu kuirudisha klabu mikononi mwa wanachama.
" licha ya kuomba kutoongeza mkataba wangu, najua changamoto za ofisi hii hivyo nipo tayari kuwasaidia kwa mawazo na changamoto zozote zile pale watakaponihitaji" Kaaya

No comments:
Post a Comment