We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Wednesday, July 10, 2019

Magufuli alivyosimamisha daladala, abiria wafunguka Mimi ni CHADEMA ila nimefurahi (+video)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli amewataka madereva wanaoendesha vyombo vya usafiri wa abiria kuzingatia sheria na taratibu za usalama wa barabarani wakati wote wa safari zao.
Rais Magufuli amesema hayo leoJuly 10, 2019 Kijijii cha Kihanga, Wilaya ya Karagwe Mkoani Kagera alipokutana na abiria na dereva wa basi dogo linalofanya safari zake kati ya Bukoba na Karagwe.
Ameeleza kuwa ajali nyingi za barabarani husababishwa na ukiukwaji wa sheria na taratibu za usalama barabarani na kwamba jukumu la kuhakikisha sheria na taratibu hizo zinatekelezwa lipo mikononi mwa watumiaji wote wa barabara hasa madereva wanaoendesha vyombo vya usafiri.
“Poleni na safari ndugu zangu, nimefurahi kuwaona na kuwasalimu, na wewe dereva hongera kwa kazi, fanya kazi zako kwa kuzingatia sheria na taratibu za usalama barabarani, pia kumbuka kusali kabla na baada ya safari” Rais Magufuli 
Kwa baadhi ya abiria hao ambao ni wanafunzi, Rais Magufuli amewataka kusoma kwa juhudi na kufanya vizuri katika masomo yao.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list