Yanga inatarajiwa kucheza mchezo wa nne wa kirafiki kesho Jumamosi dhidi ya mabingwa wa Burundi, Aigle Noir.
Ikiwa kambini mkoani Morogoro, Yanga itacheza mechi hiyo ambayo itakuwa ni ya kwanza kukutana na timu kutoka nje ya nchi.
Mratibu wa Yanga, Hafidh Saleh amesema bado kocha wao msaidizi Noel Mwandila anahitaji mechi za kirafiki kukipima kikosi chake.
Saleh amesema mchezo huo utapigwa uwanja wa Highland Park ambao Yanga inautumia kwa mazoezi ambapo mabingwa hao tayari wametua Morogoro.
Aidha, Hafidh amesema pia kuna uwezekano mkubwa siku ya Jumapili Yanga itacheza na Mawenzi Market inayoshiriki ligi daraja la pili
Noir tangu watue nchini wamecheza mechi tatu za kirafiki dhidi ya Namungo FC, Kagera Sugar na Mtibwa Sugar walipoteza mbili na kutoa sare moja.
Timu hiyo awali ilifungwa na Namungo kisha kupokea tena kipigo kutoka Kagera zote wakifungwa mabao 3-0 kabla ya kutoa sare ya mabao 2-2 dhidi ya Mtibwa Sugar.

No comments:
Post a Comment