Manara ameonekana wiki hii akiwa na wasanii mbalimbali wa Bongo Movie visiwani Zanzibar jambo lililoisukuma Mwananchi kutaka kujua sababu.
Akizungumza na Mwananchi leo Ijumaa Julai 26,2019, Manara ambaye amekuwa msemaji wa Simba ambao ni mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania 2018/19 kwa miaka zaidi ya minne sasa, amesema yupo visiwani huko wakipika filamu.
“Niliombwa na mtandao wa Swahiliflix ambao utaanza kusambaza kazi za filamu za bongo hivi karibuni kutengeneza maudhui kwa kuniona nafaa, ndio maana mmeniona niko huku Zanzibar tukilikamilisha hilo,” amesema
Alipoulizwa kama mkataba wake Simba haumnyimi kufanya hayo, anesema kufanya kwake kazi Simba hakumzuii kufanya mambo mengine.

No comments:
Post a Comment