We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Monday, July 8, 2019

Lema awataka Viongozi wastaafu kukemea tuhuma za utekaji


Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema amewataka viongozi wastaafu kukemea vitendo vya utekaji vinavyodaiwa kuendelea nchini.

Lema amesema kuwa anaamini kuwa  siku Ridhiwan akitekwa Mh. Kikwete ataongea au Abdullah akitekwa Rais Mwinyi ataongea na kuthibitisha kuwa uzee ni hekima na utu.

"Viongozi wastaafu kemeeni utekaji unaondelea Nchini.Naamini siku Rizwan akitekwa,Mh Kikwete utaongea au Abdulah akitekwa bila shaka Rais Mwinyi atathibitisha kuwa Uzee ni hekima na utu.Vunjeni ukimya,hawa wauni hawana aibu,wanaweza kumteka hata Mama Maria Nyerere. Amka paza sauti," Lema amesema kupitia ukurasa wake wa Twitter.

Hivi karibuni kumekuwa na tuhuma za kudaiwa kutekwa kwa Msaidizi wa Benard Membe Ndg Allan Kiluvya na Raphael Ongangi aliyedaiwa kutekwa na akapatikana akiwa Mombasasa Kenya.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list