Beki kisiki wa zamani wa klabu ya Simba, Jamhuri Kihwelo (Julio) ameoneshwa kukuna na usajili wa Ibrahim Ajib wa kurudi kunako Wekundu hao wa Msimbazi kwa kumwagia sifa kuwa ni moja ya wachezaji wenye uwezo mkubwa Tanzania.

Julio amesema kuwa kwa mchezaji kama Ajib na Haruna Moshi ni moja ya wachezaji wenye uwezo mkubwa hapa Tanzania, Pengina kuliko hata Samatta ila ni kujitambua tu ndio kuna mfanya Samatta aonekani ana kipaji kuwazidi wachezaji hao.
“Nikwambie tu kwa hapa Bongo hakuna wachezaji wenye vipaji kama Haruna Moshi na Ajibu. Hata Samatta hana kipaji kikubwa kama Ajib ila sema anajitambua.“Amesema Julio kwenye mahojiano yake na gazeti la Habari Leo.
Kwa upande mwingine, Julio amemtabiria makubwa Ajib ndani ya klabu yake mpya ya Simba SC, Na kumshauri aache uvivu kwenye mazoezi kwani bado anauwezo mkubwa wa kufikia ndoto zake.
Ajib alijiunga na Yanga SC misimu miwili iliyopita akitokea Klabu ya Simba na baadae kurejea tena Msimbazi. Msimu uliopita Ajib amehusika kwenye magoli 25 huku akimaliza msimu kwa kufunga magoli 6 nyavuni.
No comments:
Post a Comment