We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Wednesday, July 24, 2019

Kesi ya kupinga sheria ya ndoa yaunguruma

Rufaa ya kesi ya kupinga sheria ya ndoa ya mwaka 1971, iliyofunguliwa na Mkurugenzi wa taasisi ya Msichana Initiative Rebecca Gyumi, leo Julai 24 imeanza kusikilizwa katika mahakama ya Rufani ya Tanzania.

Katika kesi hiyo ambayo Serikali ilikata rufaa baada ya upande wa mashtaka kushinda, Wakili wa Serikali Mkuu Mark Mlwambo, amesema sheria ya ndoa ya mwaka 1971, haina madhara kwa mtoto wa kike na inapaswa kuendelea kutumika.
Akizungumza mbele ya jopo la Majaji watatu wa Mahakama ya Rufani, wakiongozwa na Jaji Augustine Mwarija, Wakili wa upande wa mashtaka Jebra Kambole, amesema Sheria hiyo ni kandamizi, inadhalilisha na kuchochea  ukatili wa kijinsia.
Kwa upande wake Rebecca Gyumi amezibainisha sababu zilizomsukuma kupinga sheria hiyo.
''Nilifungua kesi hiyo kwa sababu ya ukweli kuwa, suala la watoto wa kike kuolewa kabla ya umri limekuwa ni kubwa sana katika nchi yetu na ukiangalia takwimu mbalimbali zinazoongelea ndoa za utotoni zinaeleza kuwa, wasichana wawili kati ya watano wanaolewa kabla ya kufikisha miaka 18'' amesema Rebecca Gyumi.
Rebecca ameongeza kuwa, ndoa za utotoni ni ndoa ambazo zimekuwa zikiwaletea athari za kiafya na kielimu mabinti wengi, kwani hushindwa kutimiza ndoto zao na kwamba alifungua shauri hilo ili kuangalia ni namna gani, itaweza kuondoa ubaguzi wa umri wa mtoto wa kike kuolewa pamoja na kulinda maslahi mapana, yaliyopo kati ya mtoto wa kike na wa kiume.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list