Katika Maelezo yake katika ukurasa wa Twitter Tajiri huyo ameeleza kushukuru kwa Jezi ya Arsenal waliyomtumia huku akieleza kuwa anaangalia namna ya kushirikiana na kuikaribisha Tanzania timu hiyo Bora kutoka Ligi kuu nchini Uingereza
“Thank you @Arsenal for the signed kit! I look forward to exploring avenues for partnership with@SimbaSCTanzania. We look forward to having you in Tanzania soon. Karibu”
Baada ya kuweka ujumbe huo umeibua hisia mbalimbali miongoni mwa Mashabiki wa soka na wafuasi wake katika mtandao wa Twitter ambao wamekuwa na maoni tofauti huku wengine wakitamani kujua kama kuna ushirikiano unaokuja baina ya Timu hizo mbili.
Timu ya Simba ipo ambayo MO ndiye mwekezaji mkubwa kwa sasa ipo katika usajili wa kuboresha kikosi chao ambapo wamekuwa wakitangaza majina mbalimbali ya wachezaji wapya watakaojiunga na kikosi hicho ambapo mpaka sasa katika majina waliyotangaza tayari wamesajili wachezaji watatu raia wa Brazil.
No comments:
Post a Comment