We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Thursday, July 25, 2019

"Hata mkiniua leo hamuwezi kupona'' - Mpina

Waziri wa Mifugo na Uvuvi Luhaga Mpina, ametangaza kiama kwa wavuvi haramu waliohusika katika mauaji ya watu wanne, akiwemo ofisa mfawidhi wa rasilimali za uvuvi kanda ya Ukerewe yaliyotokea hivi karibuni.


Waziri Mpina amesema hayo, wakati akiongoza waombolezaji kuaga mwili wa Ofisa Mfawidhi aliyeuawa katika mapambano kati ya wananchi na maofisa wa kikosi cha kupambana na uvuvi haramu wa kanda hiyo.
''Natangaza vita haramu, vita mpya na tutawasaka kila mahali, tutaimarisha sekta zote kuhakikisha uvuvi haramu unakomeshwa na hata mkiniua leo atateuliwa waziri mwingine, hamuwezi kupona kwa kutumia nguvu'' amesema Mpina.
Waliofariki katika mapambano hayo ni Ofisa Mfawidhi wa rasilimali za uvuvi kanda ya Ukerewe, Ibrahim Nyangali (38), na wakazi wa kisiwa hicho ambao ni,  Damian Joseph (18), Malanja Malima (18) na Chrisant Christian (47).
Aidha Waziri amesema wavuvi haramu hawawezi kushindana na Serikali na alitangaza kuanza oparesheni ya kuwasaka wavuvi haramu iliyoanza  jana Julai 24.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list