We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Friday, July 26, 2019

GSM YAIPA YANGA GARI LA KISASA WIKI YA MWANANCHI

KATIKA kuelekea kilele cha Wiki ya Mwananchi ya Yanga iliyopewa kauli mbiu ya Funga Kazi, Kusanya Kijiji, Kampuni ya GSM imeipa timu hiyo gari la kisasa lenye TV kila upande. Wiki hiyo ya Mwananchi kilele chake kinatarajiwa kuwa Agosti 4, mwaka huu ambako Yanga watacheza mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya wababe wa Everton ya Uingereza, Kariobang Shark’s ya nchini Kenya.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Katibu Mkuu wa Kamati hiyo ya maandalizi ya Wiki ya Mwananchi, Deo Mutta, alisema kuwa gari hilo lipo katika hatua za mwisho za matengenezo. Mutta alisema kuwa, gari hilo maalum litatumika kukusanya kijiji kwa kupita baadhi ya mitaa nchini kwa wiki nzima, kuelekea kilele cha Wiki ya Mwananchi.

“Gari maalum litakalotumika kukusanya kijiji kwa kupita mitaani kwa wiki nzima kuelekea kilele cha Wiki ya Mwananchi, sasa lipo kwenye hatua za mwisho.
“Wanayanga wa Dar na mikoa ya jirani kaeni mkao chanya wa kukusanyika ili kupata ujumbe shehenevu kupitia kwa wasanii mbalimbali watakaokuwa kwenye gari hilo maalum la kisasa ambalo litakuwa na ‘screen’ kubwa kila upande utakaokuwa unaonyesha matukio mbalimbali ya Klabu ya Yanga litakapokuwa linapita mitaani na mikoani kwetu.

“Mikoa ya Dar es Salaam, Pwani na Morogoro tujitokeze kwa wingi wakati litakapokuwa linapita mitaani,” alisema Mutta

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list