Beki wa kushoto wa Yanga Gadiel Michael amekanusha tetesi zinazomuhusisha kujiunga na Simba akisisitiza hajawahi kufanya mazungumzo na kiongozi yeyote wa Simba
Inaelezwa Gadiel amekuwa akiwapiga chenga viongozi wa Yanga akiwa bado hajasaini mkataba aliopewa kabla ya safari ya Misri
Gadiel amesema mazungumzo ya mkataba mpya na uongozi wa Yanga yamekwenda vizuri na atasaini atakaporejea jijini Dar es salaam kulingana na makubaliano aliyofikia na Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya Yanga Frank Kamugisha ambaye alikuwa Misri kumaliza usajili wa baadhi ya wachezaji
Mapema leo Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla alimtaka beki huyo asaini mkataba kabla ya Ijumaa ya wiki hii vinginevyo anaweza kuondolewa kikosini
Yanga tayari imeanza mchakato wa kusaka mbadala wake ambapo baadhi ya wachezaji wanaofuatiliwa ni Erick Rutanga (Rayon Sports), David Luhende (Kagera Sugar) na Shafiq Batambuze ambaye ni mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba Gor Mahia

No comments:
Post a Comment