Amesema hayo leo Jumanne Julai 9, 2019 kwenye kongamano la amani linalofanyikia kwenye Maonyesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (DITF) maarufu sabasaba jijini Dar es Salaam, Tanzania.
Dk Tulia amesema taifa bora ni lile linalolinda na kuthamini amani na kuthamini uhuru wa wengine pasi na kuwaumiza wengine.
Amesema uhuru wa mtu unaishia kwenye pua yake na ukizidi hapo unamuumiza mtu mwingine kwa kumfanya akose amani binafsi na kuiweka nchi kwenye taharuki.
"Tunataka nchi ikue zaidi kwenye taswira ya viwanda tusingependa watu wanaochochea machafuko" amesema.
Amefafanua miongoni mwa wananchi wapo wanaovunja amani na hawataki nchi iwe na amani.
"Tujiepushe na hayo ili tusitumbukie kama taifa kwenye vitendo vya uvunjifu wa amani, tuna nafasi ya kuwafundisha watoto wetu umuhimu wa amani," amesema.
Dk Tulia amewaasa kwenye jukumu la kuhudumia wananchi wawahudumie kwa namna ambayo hawatakosa amani.
Ameeleza iwapo kuna huduma wanahitaji inayowezekana kupatikana leo ipatikane badala ya kuambiwa warudi kesho na kuwa na vinyongo mioyoni mwao.
"Usipomuhudumia ipasavyo akakosa amani, atawafanya na wengine kuikosa pia" amesema.

No comments:
Post a Comment