We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Monday, July 29, 2019

CAF imezidi kuonesha imani na waamuzi wa Tanzania, imeteua wanne

Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeteua Waamuzi Wanne (4) na Makamishna Wawili(2) kutoka Tanzania kusimamia mechi za Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho, mwamuzi Elly Sasii atasimama katikati kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa kati ya Aigle Noir ya Burundi na Gor Mahia ya Kenya utakaochezwa Uwanja wa Prince Louis Rwagasore nchini Burundi August 11 2019.
.
Sasii atasaidiwa na Mwamuzi msaidizi namba 1 Frank Komba,Mwamuzi msaidizi namba 2 Ferdinand Chacha,Mwamuzi wa Akiba Emmanuel Mwandembwa na Kamishna wa mchezo anatokea Rwanda,Gaspard Kayijuka, aidha Mtanzania Ahmed Mgoyi atakua Kamishna wa mchezo wa marudiano Ligi ya Mabingwa Gor Mahia dhidi ya Aigle Noir utakaochezwa kati ya Agosti 23,24 na 25 nchini Kenya.
.
Naye Mtanzania Khalid Abdallah ameteuliwa kuwa Kamishna wa mchezo wa Kombe la Shirikisho kati ya Proline FC ya Uganda na Master Security Services ya Malawi utakaochezwa Uwanja wa Kampala Startimes nchini Uganda.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list