Mamlaka ya utawala wa kijeshi nchini Sudan imeamuru shule zote nchini humo kufungwa kuanzia leo Jumatano ya Julai 31.
Shule zote nchini humo zinafungwa kutokana na mauaji ya watu watano wakiwemo wanafunzi wanne waliouwawa kwa kupigwa risasi wakati wa mkutano siku ya Jumatatu ya Julai 29, 2019, ambapo amri imetolewa kwa Magavana wa majimbo yote kufunga shule za watoto wadogo, msingi, na sekondari, mpaka yatakapotolewa maelekezo mengine.
Mamia ya watoto, wengi wao wakiwa kwenye sare za shule waliingia kwenye mitaa mbalimbali ya mji wa Khartoum, Jumanne, Julai 30 na kupeperusha bendera ya Sudan wakipinga kitendo cha wanafunzi wenzao kupoteza maisha.
Aidha katika mauaji hayo, watu kadhaa walijeruhiwa kufuatia waandamanaji waliokuwa wakipinga kupanda kwa bei ya mafuta na upungufu wa mkate kufyatuliwa risasi na watu wenye silaha katika eneo la El-Obeid nchini humo.
No comments:
Post a Comment