Mwenyekiti wa klabu ya Yanga Dk Mshindo Msolla kwa kushirikiana na Kamati ya Utendaji, amewateua Wajumbe 10 kuunda Kamati mpya ya fedha na mipango
Miongoni mwa walioteuliwa ni mchezaji wa zamani wa Yanga ambaye kwa sasa ni mchambuzi mahiri wa soka Ally Mayay Tembele
Kamati hiyo itaongozwa na Mwenyekiti Arafat Haji, Makamu Mwenyekiti Shija Richard huku Deo Mutta akiwa Katibu
Wajumbe ni Said Kambi, Ally Mayay, Pindu Luhiyo, Baraka Katemba, Suma Mwaitenda, Haruna Batenga na Ivan Tarimo
No comments:
Post a Comment