Nahodha mpya wa Yanga Papi Tshishimbi amesema ni heshima kubwa kwake kuwa kiongozi wa wachezaji wa timu hiyo yenye historia ya kipekee nchini Tanzania
Tshishimbi ameteuliwa kuwa nahodha wa Yanga, akichukua nafasi ya Ibrahim Ajib ambaye amesajiliwa na Simba
"Ni heshima kubwa kuwa nahodha wa Yanga. Nafurahi kupata nafasi hii," amesema
"Nitashirikiana vizuri na wachezaji wenzangu, nimefurahi kuwa nao wameunga mkono uteuzi wangu"
Kocha Mkuu wa Yanga Mwinyi Zahera alimtangaza Tshishimbi kuwa nahodha mpya huku Mrisho Ngasa akikaimu nafasi ya nahodha msaidizi inayoshikiliwa na Juma Abdul ambaye bado hajaingia kambini
Hata hivyo Zahera amesema Abdul ataendelea kuwa nahodha msaidizi atakaporejea kikosini baada ya kumalizana na uongozi wa Yanga
No comments:
Post a Comment