Uongozi wa Yanga umeamua kutotangaza hadharani majina ya wachezaji walioachwa na timu hiyo kuelekea msimu mpya wa ligi kuu ya Tanzania Bara
Mwenyekiti wa Yanga Dk Mshindo Msolla amewaambia waandishi wa habari kuwa wameshawapatia barua wachezaji wote ambao hawako kwenye mipango ya Mwalimu kwa ajili ya msimu ujao
Kuepusha sintofahamu miongoni mwa wachezaji hao, wameona sio busara kuwatangaza hadharani lakini kila kitu kitafahamika wakati kikosi cha timu hiyo kitakapotangazwa
Wengi walikuwa na shauku ya kuwafahamu wachezaji hao lakini uongozi wa Yanga umetumia busara kwa kutowatangaza mbele ya waandishi wa habari
Katika hatua nyingine, Dk Msolla amesema usajili wa Yanga umekamilika kulingana na mapendekezo yaliyotolewa na kocha Mwinyi Zahera
No comments:
Post a Comment