We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Friday, June 28, 2019

Wizara ya fedha Tanzania yasema haitoi mikopo


Wizara ya Fedha na Mipango nchini Tanzania, imekanusha habari inayozunguka kwenye mitandao ya kijamii ikiwamo Facebook kuwa inatoa mikopo  bila riba ya kilimo na biashara.

Kanusho hilo limetolewa leo Ijumaa Juni 28, 2019 na Msemaji wa Wizara ya Fedha na Mipango, Ben Mwaipaja baada ya kusambaa taarifa inayoonyesha wizara hiyo imeungana na taasissi nyingine kutoa mikopo kwa wakulima na wafanyabiashara bila riba.
Taarifa hiyo iliyopo kwenye mfumo wa picha inaeleza wizara ya fedha imeungana na taasisi binafsi iitwayo Global Entrepreneurship Forum na benki ya dunia kutoa mikopo hiyo.
"Hii taarifa ni ya uongo tunaomba muwafahamishe Watanzania kuwa haijatoka kwetu wala hakuna suala kama hilo. Inawezekana ni mbinu mpya za matapeli wanataka kujipatia fedha kwa njia za udanganyifu" amesema Mwaipaja.

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list