Misri imemrejesha kikosini Amr Warda siku mbili baada ya kumtimua kutokana na utovu wa nidhamu
Warda alikosa mchezo dhidi ya DR Congo lakini adhabu yake imepunguzwa na ataweza kushiriki michezo ya hatua ya mtoano
Kiungo huo amewaomba radhi mashabiki, marafiki, wachezaji wenzake na familia
Inaelezwa nyota Mohammed Salah ndiye aliyemuombea msamaha Warda ambapo mapema leo kupitia kwenye ukurasa wake wa Twitter, Salah aliandika;
"Tunapaswa kuamini katika nafasi ya pili, tunapaswa kuelekezana na kufundishana. Adhabu pekee sio suluhu"
Warda aliondolewa kikosini baada ya video inayomuonyesha akiwadhalilisha wanawake kwenye mtandao wa kijamii kuvuja
No comments:
Post a Comment