Makonda amesema hayo mchana wa leo Ijumaa jijini Cairo kwamba kila Mtanzania alikuwa na imani ya kupata ushindi katika mchezo wa jana dhidi ya Harambee Stars ambapo Stars ilifungwa bao 3-2.
Makonda amesema Watanzania wanapaswa kuendelea kuiombea timu yao na kuiunga mkono kwani matokeo hayo ni sehemu ya mchezo.
Makonda amesema Watanzania wanapaswa kuendelea kuiombea timu yao na kuiunga mkono kwani matokeo hayo ni sehemu ya mchezo.
Mkuu huyo wa Mkoa wa Dar es Salaam amesema licha ya Stars kupoteza ameridhika na jinsi kikosi hicho kilivyocheza kwa nguvu ikiwa ni tofauti na mchezo wa kwanza waliofunga na Senegal bao 2-0.
Amesema matokeo yaliyopatikana yamewaumiza pia wachezaji ambao walikuwa na malengo mbalimbali za kujitafutia soko la kununuliwa na timu kubwa.
Aidha Makonda amesema bado kuna nguvu kubwa ya kuiwezesha timu hiyo inatakiwa kufanyika kuijenga zaidi Stars.
Wakati huo huo, Makonda amesema Kenya kuifunga Stars kumetokana na mambo mengi ambayo baadhi ya wachezaji wa timu pinzani walitumia mbinu chafu kwa kuwaumiza mastaa wa Stars wakiwemo Simon Msuva na Mbwana Samatta.
No comments:
Post a Comment