Dk Bulamile ameyasema hayo leo Alhamisi Juni 27, 2019 jijini Dar es Salaam wakati wa mafunzo kwa waandishi wa habari kuhusu majukumu ya bodi hiyo katika kusimamia ujenzi wa majengo bora na salama kwa umma.
Amesema ramani za majengo zinatengenezwa baada ya mtaalamu (mbunifu majengo) kufika kwenye ardhi husika ambako jengo hilo litajengwa ili kuona ardhi yake, kama kuna mkondo wa maji au upepo unavuma kuelekea upande gani.
"Kisheria ni kosa kuuza michoro ya majengo, kwa hiyo tunashauri watu wasinunue michoro mitaani bali wawaone wabunifu majengo. Hii ni kwa ajili ya usalama wa nyumba zao na ujenzi unaofuata mpangilio," amesema mwenyekiti huyo.
Dk Bulamile ameongeza ni kosa kisheria kujenga jengo bila kuwatumia wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi.
Amesema katazo hilo la kisheria linawahusu wanaojenga nyumba zenye thamani ya zaidi ya Sh150 milioni au majengo yanayotumiwa na watu wengi kama vile shule, kanisa au msikiti.
No comments:
Post a Comment