Msanii wa Bongo Fleva, Timbulo anayefanya vizuri hivi sasa na ngoma ya 'Nashukuru', amezungumzia utata unaenea kuhusu malipo ya ngoma hiyo ambayo amefanya na Jux.
Taarifa zinaelea kuwa Timbulo alilipia kolabo hiyo na Jux, ambapo mwenyewe amegoma kuweka wazi kama ni kweli alifanya hivyo.
Kupitia eNewz ya EATV, Timbulo amesema kuwa mambo hayo ni ya siri na kama ni masuala ya kibiashara ni yeye na msanii husika kwahiyo hawezi kusema chochote.
"Kama watu wanakubaliana basi wanafanya, mimi sipo huko na sipo katika hizo habari"
Mtazame hapa chini akizungumzia zaidi.
No comments:
Post a Comment