Kiwango alichoonyesha mshambuliaji Emmanuel Okwi kwenye michuano ya AFcon 2019, kimewafanya mabosi wa Simba kufanya jitihada za kumbakisha Msimbazi
Okwi ameifungia Uganda mabao mawili kwenye michuano hiyo inayoendelea nchini Misri
Hatma ya mshambuliaji huyo inatarajiwa kufahamika ndani ya siku mbili kwani Simba inapaswa kutuma majina ya kikosi chake kwa ajili ya michuano ya ligi ya mabingwa tarehe ya mwisho ikiwa Jumapili ya Juni 30
Juzi Okwi aliwaambia waandishi wa habari kuwa anafurahia sapoti anayoipata kutoka kwa mashabiki wa Simba na akasema jambo lolote linaweza kutokea
Akimaanisha kwamba upo uwezekano wa kusaini mkataba mpya wa kuendelea kubaki Msimbazi
No comments:
Post a Comment