Uongozi wa klabu ya Simba uko 'busy' kukamilisha usajili wa kikosi chake kwa ajili ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika msimu ujao
Dirisha la usajili wa michuano ya CAF linafungwa leo na timu zote zitakazoshiriki michuano hiyo msimu ujao, zinapaswa kuwasilisha vikosi vyao
Nyota kadhaa wa kigeni wamewasili nchini kumalizana na Simba ambapo huenda kesho usajili wa nyota hao ukawekwa hadharani
Usajili wa Simba unaoendelea sasa umelenga zaidi michuano ya ligi ya mabingwa
Kutokana na sababu hiyo, Simba imesajili nyota kutoka sehemu mbalimbali ndani na nje ya Afrika
Nyota watatu mabeki Tairone Santos da Silva, Gerson Fraga Vieira na mshambuliaji Wilker Henrique wamesajiliwa kutoka Brazil
Kiungo Sharif Elden Shiboub ametua kutoka nchini Sudan
Wachezaji wa ndani ambao wamesajiliwa ni mlinda lango Beno Kakolanya, beki Kennedy Juma, winga Miraji Athumani na kiungo Ibrahim Ajib
No comments:
Post a Comment