Mshambuliaji wa TP Mazembe Deo Kanda aliyewasili jijini Dar es salaam juzi, anajiunga na Simba kwa mkopo wa mwaka mmoja
Klabu ya TP Mazembe imethibitisha kuwa Kanda amesafiri kuja nchini kujiunga na Simba, mabingwa wa Tanzania Bara
Kanda mwenye umri wa miaka 30 alijiunga na Mazembe kwa mara ya kwanza mwaka 2010 baadae kuondoka kisha kurejea tena
Miongoni mwa mataji makubwa aliyotwaa akiwa Mazembe ni taji la ligi ya mabingwa huku akipata nafasi ya kucheza michuano ya kombe la dunia la vilabu mwaka 2015 akiwa sambamba na akina Mbwana Samatta
Mshambuliaji huyo anatajwa kutua nchini kuchukua nafasi ya Okwi ambaye bado amekuwa mgumu kusaini mkataba kuendelea kubaki Msimbazi
No comments:
Post a Comment