We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Sunday, June 30, 2019

Stars yasubiri muujiza dhidi ya Algeria, inaweza kusonga mbele

Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Jumatatu itakamilisha safari yake ya ushiriki wa michuano ya Afcon 2019 kwa kuumana na Algeria katika mchezo utakaopigwa saa nne usiku
Mchezo huo utapigwa wakati mmoja na mchezo mwingine wa kundi C kati ya Kenya dhidi ya Senegal
Miujiza inaweza kuibeba Tanzania inayoshiriki michuano ya Afcon kwa mara ya pili, kutinga hatua ya mtoano kama itaifunga Algeria huku Kenya ikipoteza dhidi ya Senegal
Kuelekea mchezo huo Watanzania wanapata matumiani japo yanaweza kuwa madogo kutokana na ukweli kwamba watachuana na Algeria ambayo tayari imefuzu hatua ya mtoano
Kwa Algeria mchezo huo utakuwa wa kukamilisha ratiba tu
Lakini hali ni tofauti kwa majirani zao Kenya ambao watacheza na Senegal ambayo inahitaji kushinda ili kujihakikishia nafasi ya kutinga hatua ya mtoano ambayo ni hatua ya 16 bora
Algeria inaongoza kundi C ikiwa na alama sita baada ya kushinda michezo yote miwili
Inafuatiwa na Senegal yenye alama tatu sawa na Kenya lakini Senegal ikiwa na uwiano mzuri wa mabao
Tanzania haina pointi lakini kama itapata ushindi mnono dhidi ya Algeria na Kenya kupoteza dhidi ya vigogo namba moja barani Afrika Senegal, inaweza kupenya hatua ya mtoano kupitia 'best looser'

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list