Yanga ndio timu iliyokuwa 'busy' zaidi kwenye dirisha la usajili lililofunguliwa Juni 15 likitarajiwa kufungwa Julai 31 kwa ligi kuu ya Tanzania Bara wakati lile la CAF likifungwa kesho Juni 30 2019
Yanga imefanikiwa kusajili nyota wapya 13 na inaendelea kuwaongezea mikataba nyota wake waliopendekezwa kubaki na kocha Mwinyi Zahera
Kwa usajili uliofanywa, kikosi cha Yanga kitakuwa na mabadiliko makubwa na hii ndio sababu uongozi wa timu hiyo umepanga kuanza kambi ya maandalizi ya msimu mpya mapema
Wachezaji wote waliosajiliwa wanatarajiwa kuanza kurejea wiki ijayo ili Julai 07 waanze rasmi maandalizi ya msimu mpya
Kocha Mwinyi Zahera anaweza kurejea mapema kuungana nao akiambatana na wachezaji wanaoshiriki fainali za Afcon ambao timu zao zitashindwa kusonga mbele hatua ya mtoano
Nyota wapya waliokamilisha usajili Yanga
1. Farouq Shikalo
2. Metacha Mnata
3. Ally Ally
4. Ally Mtoni
5. Lamine Moro
6. Mustapha Suleyman
7. Patrick Sibomana
8. Issa Bigirimana
9. Mapinduzi Balama
10. Abdulaziz Makame
11. Maybin Kalengo
12. Juma Balinya
13. Sadney Urikhob
No comments:
Post a Comment