We are currently working on a new website.
Stay tuned for more information.

to stay updated on our progress.

Friday, June 21, 2019

NIYONZIMA, OKWI, JUUKO, ZANA, ASANTE KWASI, KOTEI NA GYAN MBIONI KUTEMWA SIMBA

Uongozi wa Simba uko kwenye michakato ya kukamilisha usajili ambapo jana ulimtambulisha kiungo wa kigeni kutoka Sudan Sharaf Eldin Shiboub aliyesaini mkataba wa mwaka mmoja
Inaelezwa kuna nyota wengine wanne ambao tayari wako nchini kumalizana na mabingwa hao wa Tanzania Bara
Taarifa ambazo zimeripotiwa na baadhi ya magazeti leo zinadai Simba imeamua kuachana na 'maproo' saba ambapo miongoni mwao wamo viungo Haruna Niyonzima na James Kotei
Wengine ni Zana Coulibaly, Nicholas Gyan, Emmanuel Okwi, Juuko Murshid na Asante Kwasi
Nyota wa kigeni waliobaki ni Meddie Kagere, Clatous Chama na Paschal Wawa
Baadhi ya nyota wameachwa baada ya mikataba yao kumalizika huku wengine wakitupiwa virago kutokana na kutokidhi vigezo vinavyohitajika kuendelea kubaki Msimbazi
Kwa upande wa Okwi ni suala la maslahi, awali ilielezwa kuwa Mganda huyo atasaini mkataba mpya baada ya kumaliza michuano ya Afcon inayoanza leo huko Misri
Aidha wachezaji ambao usajili wao umekamilika ni Beno Kakolanya, Sharif Eldin Shiboub, Miraji Athumani, Kennedy Juma na Ibrahim Ajib
Simba pia iko katika hatua za mwisho kukamilisha usajili wa mlinzi wa kati raia wa Brazil Gerson Viera pamoja na nyota wengine wawili wa kigeni ambao tayari wako jijini Dar es salaam kusaini mikataba
Mwenyekiti wa Simba Swedi Mkwabi amesema wachezaji wapya watakaosajiliwa na timu hiyo hawatazidi saba

No comments:

Post a Comment

Powered by Blogger.

Report Abuse

About Me

TAARIFA MPYA KUHUSU APP YETU KAMA BADO HUPATI HABARI ZETU

Habari!! Ni kipindi cha takribani wiki 1 kimepita ukiwa hupati habari, tunaomba radhi kwasababu tumekuwa tukifanya maboresho zaidi. Leo ...

Total Pageviews

Search This Blog

Blog Archive

Labels

Mobile Logo Settings

Mobile Logo Settings
image
recent/hot-posts

Random Posts

3/random/post-list

Recent Posts

3/recent/post-list